Mtoto wa Rais wa Marekani Aliyeanguka na Ndege na Kufa Kisa Mawenge

Miaka 20 iliyopita #John F #Kennedy #Jr (Mtoto pekee wa Rais wa 35 wa Marekani #JFKennedy) alianguka baharini na ndege yake binafsi ndogo aina ya #Piper #Saratoga na kupoteza maisha yake, mchumba wake #Carolyn na shemeji yake #Laurian ambaye ni dada wa mchumba wake.

Taarifa zinasema Kennedy jioni hiyo alirusha mwenyewe ndege yake akiwa na mchumba wake na shemeji yake wakati mwalimu wake aliyekuwa anamfundisha urubani aliombwa kuungana nao lakini alikataa kwenda kwasababu alikuwa na dharura.

Taarifa zaidi zinasema Kennedy alikuwa na leseni ndogo binafsi ya kurusha ndege "Private Pilot License" #PPL ila hakumalizia mafunzo ya kurusha ndege katika hali ya hewa isiyo ruhusu rubani kuona nje #Instrumental #Flight #Rule au #IFR 'ratings' ambayo hutumia vifaa tu vilivyo mbele ya chumba chake #CockpitInstrument kumuongoza.

Ripoti ya Mamlaka husika ya uchunguzi wa ajali nchi Marekani #NTSB imesema Kennedy alikutwa na hali inayoitwa #SpartialDisiorientation ambayo rubani hushindwa kutambua ndege yake imekaa vipi angani hasa kushindwa kutambua wapi juu na wapi chini au kuhisi ndege imelala upande wakati ipo sawa hasa pale akizongwa na hali ya hewa ya ukungu mzito au mawingu na kutoweza kuona nje hivyo kama rubani hana mafunzo ya kutosha kusoma mitambo yake mbele ya kuonesha ndege yake imekaa aje anaweza kufuata akili yake inavyodhani na kusababisha kuingiza ndege kwenye matatizo zaidi au ajali.

Ripoti ya NTSB inasema Kennedy naye alikutwa na hali hiyo hivyo akadhani anaokoa ndege kumbe anaipeleka chini baharini n kupelekea vifo vya wote watatu.

Spartial disorientation kwa mtu wa kawaida ni kama aina ya mawenge au kizunguzungu cha kuona unaanguka kumbe upo sawa.

Je, una maoni gani kuhusu ajali hii?
Usisahau Like na share
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad