Mugabe kuzikwa nyumbani kwa Baada ya Mzozo Kati ya Familia Yake na Serikali Kumalizika


Mwili wa rais wa Robert Mugabe utazikwa nyumbani kwao, baada ya mzozo kati ya familia yake na serikali kuhusu mahalia takapozikwa kuchukua mkondo mwingine.

Mugabe alifariki mwezi mapema mwezi huu akiwa na miaka 95 na ibada ya mazishi kufanyika katika mji mkuu wa Harare.

Serikali ilikua imepinga ombi la familia yake la kumzika kiongozi huyo katika eneo la Zvimba, na kushinikiza azikwe katika makaburi ya mashujaa wa kitaifa.


Familia yake hatimae ilikubali lakini serikali ikabadilisha msimamo huo siku ya Alhamisi.

Haikubainika ni nini kilichosababisha mipango ya awali ya mazishi ya Mugabe kubadilishwa.

Familia ya Mugabe ilikubali azikwe katika makaburi ya Heroes Acre baada ya makubaliano kufikiwa kuwa mnara wa makumbusho utajengwa kumuenzi kiongozi huyo wa kwanza wa Zimbabwe.

Katika taarifa iliochapishwa Alhamisi, Waziri wa Mawasiliano Nick Mangwana alisema mabadiliko hayo yanazingatia sera ya "kuheshimu uamuzi wa familia ya marehemu".

Mugabe alifariki Singapore alipokua anapokea matibabu yasaratani na mwili wake kusafirishwa nyumbani Zimbabwe.

Baada ya kifo chake familia yake ililamika hadharani kuwa haikushauriwa kuhusu mipango ya mazishi yake ya kitaifa.

Katika taarifa familia hiyo iliilaumu serikali kwa kutumia nguvu kupanga mazishi ya Mugabe katika makaburi ya mashujaa kinyume na "matakwa yake [Mugabe]".

Taarifa hiyo aidha ilisema kuwa ombi lake la mwisho lilikua la mke wake , Grace Mugabe, kutoondoka kando ya jeneza lake hadi atakapozikwa.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad