Mume Mtarajiwa wa Irene Uwoya Azua Gumzo Mitandaoni


HUKO Instagram wewe wape picha tu, maelezo watajaza wenyewe! Umbea mpya unaosambaa mitandaoni kwa sasa ni juu ya picha inayodaiwa ni ya mume mtarajiwa wa muigizaji Irene Uwoya ambaye jina lake halijafahamika.

 Picha hiyo inamuonesha Uwoya akiwa amekaa kwenye eneo ambao lina maputo huku jamaa huyo akiwa nyuma yake na mkono mmoja akiwa amemshika Uwoya shingoni kuashiria mahaba f’lani hivi ‘ameizingi’.

Hata hivyo, wambea wamehangaika wee kumjua jamaa huyo imeshindikana kwani usoni amezibwa kwa  kutumia emoji yenye kopa ndani yake.  “Jamani wambeya wenzangu tuhakikishe tunamchimba huyu hadi tumjue ni nani, sisi siyo watu wa mchezomchezo,” alichangia mmbeya mmoja Insta.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Lava lava s shauli ayako.
    Ndikumana mungu Amrehemu.
    Janjaro kaachia njiani.

    Safari ni ndefu.. Utaiweza..?

    SADC aliomba..Makonda akampotezea.
    Sasa unaweza kuona Picha . unalo mwanangu..?

    Usije ukajuta au na ww umekuwa Mheshimiwa kama yule nani vile???

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad