Mwakinyo afunguka kuhusu pambano lake la kwanza bongo



Bondia namba moja kwa Afrika kwenye uzito wa Super Welterweight kg 69 na namba 19 duniani Hassan Mwakinyo, amesema kuwa hana mashaka na mabondia kutoka Uingereza wala Marekani ambao wamekubali kupanda ulingoni kwenye pambano la World Class Fight Tanzania.

Pambano hilo linatarajiwa kufanyika Octoba 26 uwanja wa Taifa na litarushwa mubashara kwenye baadhi ya vituo vya Televishini vya Bongo na vile vya nje kutokana na heshima ya Mwakinyo.

Mwakinyo amesema kuwa anatambua kwamba Waingereza na mabondia kutoka Marekani wamepania kupambana naye jambo linalomfanya ajifue zaidi.

“Wanajua aina ya bondia wanayekwenda kupambana naye ana uwezo wa aina gani hivyo nao wanajipanga kuonyesha uwezo wao nitawaambua mapema kabisa kwani nitakuwa nyumbani na mashabiki wangu, hili litakuwa pambano langu la kwanza nyumbani ni lazima nifanye mambo makubwa.

“Kuhusu kutaja majina yao kwa sasa naliacha suala hilo kwa mashabiki, kuna majina ya mabondia kutoka nchi tano ambazo zinahitaji kupambana nami wenyewe watanichagulia nani nipande naye ulingoni, sapoti muhimu kwa mashabiki,” amesema Mwakinyo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad