Mwalimu bora duniani kutoka Kenya akutana na Donald Trump ikulu ya Marekani

Peter Tabichi kutoka Kenya, aliyetuzwa Mwalimu bora duniani mapema mwaka huu, amekutana na rais wa Marekani Donald Trump katika ikulu ya White House huku akitarajiwa kutoa hotuba katika baraza kuu la Umoja wa mataifa leo.

Brother Tabichi, ni mtawa wa shirika la kikatoliki la Mtakatifu Fransisco wa kapuchini na alishinda tuzo ya mwalimu bora duniani mnamo Machi 2019.

Anafunza sayansi katika shule ya mseto ya upili ya Keriko katika kaunti ya Nakuru, kaskazini magharibi mwa mji mkuu, Nairobi.

Picha ya Tabichi akikutana na rais Trump iliwekwa na afisa wa mawasiliano kutoka ikulu kwenye Twitter ambaye alisema Tabichi alitoa " 80% ya mshahara wake kwa mwezi kuwasaida masikini nchini mwake Kenya"

Peter, unatutia moyo sisi sote! Asante kwa uwajibikaji wako kwa wanafunzi wako." Alisema Stephanie Grisham kutoka ikulu ya Marekani.

Tabichi anatarajiwa kutoa maombi kabla ya kuanza kwa kikao cha baraza kuu la Umoja wa mataifa mjini New York baadaye leo.

Anatarjiwa pia kuzungumzia kidogo kuhusu namna alivyofanikiwa kufika alipofika katika taaluma ya uwalimu.


Brother Peter Tabichi amesifiwa kama "mwalimu wa kipekee" ambaye hugawa sehemu kubwa ya mshahara wake

Tabichi amenukuliwa kusema kwamba "Hii ni heshima kubwa kwa watawa wa St Franciscan. Inaonyesha kuwa Umoja wa mataifa unatutambua kutokana na kwamba ina jukumu kuu katika kuendeleza utu."

Katika tuzo hiyo iliotolewa katika shindano lililoandaliwa na Wakfu wa Varkey , Brother Peter aliwapiku washiriki wengine 10,000 waliochaguliwa kutoka nchi 179.

Brother Peter anasema kuna "changamoto ya ukosefu wa vifaa " katika shule yake ukiwemo uhaba wa vitabu na waalimu.

Madarasa yenye uwezo wa kuwa na wanafunzi kati ya 35 hadi 40 hulazimika kuwa na wanafunzi 70 na 80, jambo analosema linamaanisha kuwa darasa linakuwa na wanafunzi wengi kupita kiasi, na ni tatizo kwa waalimu.

Ukosefu wa intaneti ya kuaminika unamlazimisha kusafiri hadi kwenye cyber-cafe kwa ajili ya kupakua maelezo ya masomo yake ya sayansi.

Na wanafunzi wengi hutembea zaidi ya maili nne kwenye barabara mbovu kufika shuleni.

Lakini Brother Peter anasema ameazimia kuwapatia fursa ya kusoma na kufikia ndoto zao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad