Mwalimu Mkuu akamatwa tena baada ya Binti aliyemkana kukamatwa na kuhojiwa


Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma, ACP Martin Ottieno amesema tayari jana usiku wamemkamata kwa mara nyingine Mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Nyantore, Jason Rwekaza (42) ambaye aliachiwa huru na Mahakama ya Hakimu mkazi Kigoma Septemba 16 baada ya mwanafunzi kukana ushahidi alioutoa polisi mbele ya mahakama kwamba hamfahamu aliyeshiriki naye mapenzi hadi kupata mimba.

Kamanda ACP Ottieno amesema kuna jambo lililomshawishi mwanafunzi kufikia uamuzi huo na sasa wanaandaa mashtaka dhidi ya mwalimu huyo kwa makosa yanatomkabili na muda siyo mrefu watamfikisha mahakamani.

Ikumbukwe September 16 mwaka huu mahakama hiyo ya ilimwachia huru mwalimu huyo baada ya upande wa mashtaka kuomba kutoendelea na shauri hilo kufuatia shahidi wa pili mwanafunzi mwenye mimba kueleza mbele ya mahakama kuwa hamfahamu mtu aliyeshiriki naye mapenzi hadi kupata mimba.

Aidha shahidi huyo alikana kuwa na umri wa miaka 16 kama upande wa mashtaka ulivyosema kupitia upelelezi wa polisi na kwa mujibu wa baba wa mwanafunzi huyo amesema binti yake ana umri wa miaka 19 na kwa muda mrefu Polisi walikuwa wakimshawishi aseme ana miaka 16 tofauti na anavyofahamu.

Kesi hiyo kwa mara ya kwanza ilisomwa Agosti 14 ambapo shahidi wa kwanza mama mzazi wa mwanafunzi huyo Sakina Kazili (55) aliiambia mahakama hiyo Septemba 12 kuwa binti yake ana miaka 16 na kwamba alizaliwa Februari 7, 2003.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad