Mwanamke Afanyiwa Upaauaji Baada ya Kumeza Pete ya Ndoa Akiwa Kwenye Ndoto

Mwanamke mmoja nchini Marekani amefanyiwa upasuaji baada ya kyivuta peke yake ya ndoa kutoka kwenye kidole chake na kuimeza wakati alipokuwa amelala fofofo

Jenna Evans, mwenye umri wa miaka 29, amesema kuwa mchumba wake Bobby alikuwa katika treni ya mwendo kasi na akalazimika kumeza pete ili kuilinda dhidi ya "watu wabaya".

Haki miliki ya pichaJENNA EVANS/FACEBOOK
Alipoamka katika nyumba yake mjini California aligundua kuwa alichofikiria kilikuwa ni ndoto tu , lakini akagundua kuwa pete yake haipo kidoleni.

Alisema kuwa alipogundua hilo , alimuamsha Bobby kumuelezea, na ndipo wapenzi hao wakaenda hospitalini.

Mafuta yapanda bei baada ya mashambulio Saudia
Magufuli: Jimbo la Tundu Lissu lilitelekezwa
Afariki akimkwepa ndege mwenye hasira
Bi Evans anasema alihangaika kukumbuka kisa hicho ili kuwaeleza madaktari ''kwasababu nilikuwa ninacheka na kulia sana ".

Mwisho wa ujumbe wa Facebook wa Jenna
Picha za skani ya X-ray zilibaini kuwa pete hiyo ilikuwa ndani ya tumbo lake, na madaktari wakakubaliana kuwa lingekuwa si jambo la busara ''kuiacha ijiondoe tumboni yenyewe kwa njia ya choo''

Bi Evans, ambaye ni mkazi wa San Diego , baadae alifanyiwa upasuaji wa kuiondoa pete hiyo lakini alitakiwa kusaini fomu za kukubali kufanyiwa upasuaji huo, ikiwa kifo kingetokea.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad