Mwanamke Ukiona Mwanaume Amehamia Kwako na Anatabia Hizi Mfukuze Kama Mbwa Koko


Uko kwenye mahusiano, upo na mwanaume, alikua anakuambia kuwa anafanya kazi ingawa hata ulikua hujawahi kufika kazini kwake, lakini alikua kakuambia kuwa anafanya kazi, na kweli alikua anakupa vitu vidogo vidogo kama matunda, nauli baada ya mechi au hata alikua hatoi pesa lakini alikua anasema anaenda kazini kila siku. Ghafla anakuambia kuwa kasimamishwa kazi, yaani kazi yenyewe ulikua huna uhakika kama anafanya ila ghafla kasimamishwa, au kafukuzwa kabisa.

Ghafla unaona anaanza kukuomba pesa, unaona hamna shida si baby, ana matatizo, anaomba pesa unampa, ghafla anaanza kutaka umhudumie, gfhafla anataka kuhamia kwako, anakuambia kuwa chumba chake anataka kurudisha aje kwako. Ghafla wewe ndiyo kila kitu, wewe kwake ndiyo baba ndiyo mama, ndiyo mjomba ndiyo Shangazi, ndiyo mshikaji, ndiyo mbwa ndiyo paka, ndiyo mbuzi ndiyo kondoaa, yaani anaanza kukutegemea kwa kila kitu.

Hana kazi lakini hatafuti kazi, yaani akiamka asubuhi ni kwenye sofa tu, ametengeneza mpaka na kasehemu kake kwenye sofa kashaanza kutoboka, anaishi kwako lakini nyumba ishaanza kunukia harufu yake. Dada yangu huyo mtu fukuza, atakupa mimba muda si mrefu na utakua na watoto wawili, najua unajiona kama umedoda afadhali huyo ila ubaya nikuwa siku ukimfunguilia akatoka akakutana na mwanamke mwingine mwenye malezi kama yako basi jua kua na wewe utakua umeachwa! Huyo mtu hakua na kazi ila kazi yake ni kutafuta wadada wapweke kama wewe na kujifanya anawapenda!
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad