Mwanamuziki Kidum Apigwa Marufuku Kushiriki Tamasha la Rwanda


Mwanamuziki maarufu wa Burundi na Afrika mashariki Jean Pierre Nimbona maarufu Kidum amepigwa marufuku kushiriki katika Tamasha la kila mwaka linalotarajiwa kuandaliwa nchini Rwanda la Kigali Jazz Fusion.

Waandalizi wa onyesho hilo walimwambia Kidum kwamba agizo hilo linatoka kwa mamlaka ya mji wa Kigali.

Kidum amekuwa akishiriki katika tamasha za muziki nchini Rwanda kwa zaidi ya miaka 16 na anasema kwamba hajawahi kuwa na tatizo lolote.


Mnamo tarehe sita mwezi Septemba alishiriki katika ufunguzi wa klabu moja ya burudani mjini humo.

Wasimamizi wa tamasha hilo waliwaandikia mashabiki wa tamasha hilo wakisema kwamba kwa sababu zisizowezekana hatutaweza kumuons kidum katika tamasha la Kigali Jazz litakalofanyika Ijumaa tarehe 27 mwezi Septemba

Anasema kwamba marufuku hiyo anaamini huenda inatokana na uhusiano mbaya kati ya serikali ya Rwanda na Burundi.

Na muda tu alipopokea barua hiyo mwanamuziki huyo aliandika katika mtandao wake wa twitter akiwaomba msamaha mashabiki wake.

Poleni mashabiki wangu kwa sababu nisizojua inaonekana mamlaka ya mji wa Kigali haijaniruhusu kushiriki katika tamasha la mwezi huu na pengine matamasha mengine katika siku za baadaye sijui.

Nawashukuru nyinyi na mapromota kwa kunikumbuka kila mara. Mungu awabariki mashabiki wangu .

Na muda mfupi baadaye mashabiki wake walianza kuchapisha jumbe

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad