Ndege mbili Zanusurika Kupata Ajali kwa Kugongana Angani


Ndege mbili za abiria zimepigwa picha sekundi tano tu kabla ya ajali kuweza kutokea ambayo imezuiwa kwa kikosi cha maafisa wa uangalizi wa ndege , uchunguzi umebaini.



Ajali hiyo ambayo nusra ingetokea ilikuwa ni kati ya ndege aina ya Cessna 208 mnamo Aprili na iliweza kuepukika kwa “tundu la sindano”, bodi ya Airprox imesema.

Mojawpao ya ndege hizo ilikuwa imetoka kumshusha jamaa aliyeshuka kwa parashuti huko Sibson Aerodrome, karibu na Peterborough nchini Uingereza, huku ndege ya pili ilikuwa ikipelekwa na mwanafunzi aliyekuwa na mwalimu wake.

Maafisa wa Kituo cha uangalizi wa ndege waliiambia ndege iliyokuwa juu ilizunguka eneo hilo mara moja kabla ya kutua.

Bodi ya Airprox, inayochunguza matukio ya ajali ambazo huenda zingetokea imegundua kwamba ndege iliyomshusha jamaa kwenye parashuti ilikuwa inakaribia kutua mita 15 juu ya ndege hiyoya pili.


Mwalimu wa mwanafunzi rubani huyo alisikia kelele, akaona kivuli cha ndege iliyokuwa juu yao na kuchukua udhibiti wa usukani kutoka kwa mwanafunzi huyo.

Afisa mmoja kutoka kituo cha uangalizi aliiambia ndege hiyo ya juu izinguke mara nyingine tena kabla ya kujaribu kutua tena.

“Marubani wa ndege zote mbili walikuwa hawajui nafasi iliko ndege nyingine na iwapo hatungeiambia izunguke tena ilikadirwa kwamba ndege hizo zingegongana baada ya sekundi tano tu,” afisa huyo alisema.

Maafisa wa kituo cha uangalizi wa ndege wa Sibson Aerodrome wamepongezwa na bodi ya Airprox ambao ilisema walifanikiwa kuizuia ajali.

Wachunguzi wanasema ndege zote mbili zinahudumu kutoka uwanja huo wa ndege, huenda basi wangeajadiliana mipango ya safari kabla ya kuondoka.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad