Ndege Yaanguka Serengeti, Yaua Watanzania Wawili

Ndege ndogo ya Shirika la Auric Air imepata ajali leo Jumatatu asubuhi Septemba 23, 2019 katika uwanja mdogo wa ndege eneo Seronera ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti nchini Tanzania.



Ajali hiyo imetokea saa 1:30 asubuhi ambapo ilikuwa ikiruka kutoka Serengeti kwenda Arusha baada ya kushusha watalii.


Katika ajali hiyo, rubani na abiria mmoja wamefariki dunia.

Kamishna Msaidizi mwandamizi wa shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), Pascal Shelutete amethibitisha kutokea ajali hiyo.

“Tunatoa taarifa zaidi baadaye kwani sasa kazi inayoendelea ni kuokoa vitu na kuhifadhi miili,” amesema.



Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, wamedai kuwa ndege hiyo iligonga katika jengo la choo cha zamani na kuanguka huku wakieleza kuwa rubani wa ndege hiyo anmayesadikiwa kufariki anajulikana kwa jina moja la Nelson.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad