Ndugu wa marehemu watano waliofariki katika ajali Kibiti watakiwa kufika Muhimbili kufanyiwa DNA


Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) imepokea maiti tano za ajali ya gari iliyotokea Kibiti mkoani Pwani ili kufanyiwa vina saba (DNA).

Miili hiyo ni ya watu wazima wanne na mtoto mmoja imeungua sana (beyond recognition) kwamba utambuzi wake ni mgumu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma,
Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminieli Aligaesha, alieleza kuwa tayari Hospitali ya Taifa Muhimbili imefanya uchunguzi (postmortem) na kuchukua sampuli kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kitengo cha Forensic Pathology pamoja na Mkemia Mkuu wa Serikali ili kufanya uchunguzi zaidi.

“Tunawaomba ndugu wa karibu wa marehemu hawa hususani baba, mama na watoto kujitokeza kuanzia kesho tarehe 2 Septemba, 2019 saa mbili asubuhi ili kuchukuliwa sampuli na Mkemia Mkuu wa Serikali ili kusaidia kufanya uchunguzi wa kulinganisha vinasaba kati ya ndugu na marehemu na ili waweze kupewa miili hiyo kwa ajili ya mazishi baada ya uchunguzi kukamilika,” alieleza

Miili ya marehemu watano walifariki kwenye ajali ya lori la Dangote lililogongana na gari ndogo kisha kuwaka moto.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji, Onesmo Lyanga amesema miili ya watu watatu waliokuwa kwenye Lori la Dangote haijaweza kutambulika mara moja kutokana na kuteketea kwa moto.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad