Papa Aanza Ziara Rasmi Atua Msumbiji


Kiongozi wa kanisa Katoliki Duniani Papa Francis, ameanza ziara rasmi ya kihotoria Barani Afrika wiki hii - akiwa anazitembelea Msumbiji, Madagascar na Mauritius.

Umaskini, uhifadhi wa mazingira na ufisadi ni miongoni mwa mambo yanatorajiwa kuigubika ziara ya Papa katika mataifa ya Afrika.

Kando na Papa Francis, Mapapa wawili wengine wamewahi kuzuru mataifa ya Afrika. Wa kwanza alikuwa Papa Paul VI aliyezuru Uganda mwaka 1969.

Ziara hii ya Papa Francis inatazamwa kama jitihada zake ya kuwa na malengo mapya chini ya uongozi wake baada ya kashfa za miezi kadhaa kuhusu namna kesi za unyanyasaji wa kingono zilivyoshughulikiwa.

Umati wa watu waliojawa na furaha umemkaribisha Papa Francis nchini Msumbiji aalipoanza ziara yake ya mataifa matatu ya Afrika.

Papa Francis amehudhuria mkutano wa vijana wa dini mbali mbali katika Maxaquene Pavillion mjini Maputo, Septemba 5, 2019. - Papa tayari amewasili nchini Msumbiji.

Wahudumu katika kanisa katoliki wamenukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari wakisema kwamba ziara hii ambayo ni ya pili Papa Francis kuwahi kuifanya kusini mwa jangwa la Sahara Afrika, ni fursa muhimu kutoa wito mpya uliogubikwa katika barua yake ya mnamo 2015 "Laudato Si" inayuhusu kulinda mazingira.

Ongezeko la watu barani Afrika linatoa fursa kwa ukuaji wa ongezeko la waumini wa Kanisa Katoliki pia barani.

Papa anatarajiwa pia kuzuru kisiwa cha Madagascar, na tayari mabango ya kumlaki yameshamiri mitaani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad