Papa alaani rushwa ya kimataifa


Akikamilisha ziara yake ya siku mbili nchini Msumbiji, kiongozi wa Kanisa Katoliki ulimwenguni, Papa Francis, amekosoa rushwa inayofungamanishwa na misaada ya maendeleo.

Licha ya utajiri mkubwa wa mali ghafi, wananchi wengi wa nchi hiyo ya kusini mashariki mwa Afrika wanaishi katika hali ya umaskini uliokithiri, amesema kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki ulimwenguni katika misa katika mji mkuu Maputo.

Amelaani mitindo ya kufungamanishwa masilahi ya kiuchumi ya mataifa tajiri kiviwanda na misaada ya maendeleo.

Amesema mitindo hiyo inatoa picha kana kwamba wale wanaojidai wanataka kusaidia, kimsingi wanafuata masilahi mengine.

Kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni Papa Francis anatarajiwa kuondoka Maputo kuelekea Antananarivo-Madagascar-kituo cha pili cha ziara yake hiyo itakayomfikisha pia kisiwani Mauricius.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad