Papa Francis Awashutumu Wakosoaji Wake Kumfanyia Hila
0
September 11, 2019
Papa Francis amewashutumu wakosoaji wake kwa kumfanyia hila , na akasema kuwa ”haogopi” mgawanyiko katika kanisa katoliki. Akizungumza baada ya ziara yake baraniu Afrika, Papa amezungumzia suala la makasisi wenye itikadi kali za kikatoliki ambao wamekuwa wakimkosoa,
Wanaoume hao “hawalitakii mema kanisa “, bali kile wanachokijali ni ” kubadilisha mapapa, kubadilisha mitindo, kubuni matawi ya kanisa “, alisema.
Viongozi wa kanisa katoliki wa Marekani waliwahi kukosoa Papa kwa maoni yake.
Hii ni mara ya kwanza kwa Papa kuzungumzia wazi kuhusu uwezekano wa mpasuko ndani ya kanisa katoliki , ambalo lina zaidi ya wafuasi zaidi ya bilioni moja duniani.
Papa Francis alizitoa kauli zake alipokuwa ndani ya ndege iliyomrejesha Roma baada ya ziara aliyoifanya katika mataifa ya Madagascar, Mauritius na Msumbiji.
Alikuwa ameulizwa swali na mwandishi kuhusu mashambulio dhidi yake kutoka kwa viongozi mahafidhina wa kanisa Katoliki , kupitia vituo vya televisheni na tovuti za Marekani.
Baadhi ya viongozi wa Kikatoliki – hususan Marekani lakini pia katika baadhi ya maeneo mbali mbali duniani -wamemkosoa Papa kwa kuchuja imani yao , na hata wamekwishotoa wito wa kujiuzulu kwake.
Hawafurahii misimamo yake kuhusu mazingira na uhamiaji . Lakini kubwa zaidi wanapinga hatua zake za kuruhusu waliotalikiana na walioolewa kwa mara ya pili kupokea ukaristi.
“Siogopi mgawanyiko ,” alisema Papa Francis na kuongeza kuwa mengi yametokea katika historia ya kanisa Katoliki . “Ninaomba mgawanyiko usitokee , Kwasababu afya ya roho za wengi hulitegemea kanisa .”
Papa Francis samesema kuwa fikra za kisiasa zinachafua namna mitazamo ya wakosoaji dhidi yake.
“Vitu ninavyosema kuhusu masuala ya kijamii ni sawa na alivyosema Papa John Paul . Ninamnukuu na wanasema ‘ papa amezidi kuwa mkomunisti ‘,” aliwaambia maripota.
Alisifu “ukosoaji unaojenga “, lakini si “wale wanaotabasamu huku wakikufanyia hila”.
” Ukosoaji haukutoka tu Marekani bali kutoka maeneo mengine, wakiwemo Curia,” alisema, akimaanisha bodi ya utawala ya kanisa katoliki.
Katika mwaka wa 2,000-wa historia yake kanisa katoliki limegawanyika mara kadhaa na mgawanyiko unaokumbukwa zaidi ni ule wa mwaka 1054, wakati kanisa la Kiorthodox la mashariki lilijitenga kutoka kwa Roma.
Migawanyiko ilisababisha upinzani dhidi ya Papa -ambapo watu wengine waliodai kuwa mapapa na na kukataa kuukubali utawala wa Rome.
Hivi karibuni kabisa, Askofu mkuu wa Ufarasa Marcel Lefebvre aliwatawaza maaskofu wanne bila idhini ya Papa mwaka 1988.
Chanzo BBC.
By Ally Juma.
Tags