Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) taifa, Humphrey Polepole, amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita Modest Alpolnary, kutenga kiasi cha Shilingi Milioni 200 kwa ajili ya kuvisaidia vikundi vya vijana na Wanawake wa chama hicho kuanzisha viwanda.
Polepole ameyabainisha hayo wakati wa uzinduzi wa Geita ya Kijani ulioandaliwa na UVCCM Mkoani humo.
''Wote wapigwe semina, waambiwe maana ya viwanda hivyo, waambiwe namna ya fursa zilizopo, wapewe ujuzi wa namna ya kuviendesha'' amesema Polepole.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Geita Manjale Magambo,amemuomba Polepole kufikisha kilio cha vijana ambao, wamekuwa wakifukuzwa kazi na baadhi ya Migodi ya dhahabu hapa nchini na kisha taarifa zao kusambazwa kwenye migodi yote ili wasiajiliwe popote pale.