Polepole amzungumzia Cyprian Musiba


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema kuwa Mwanaharakati Huru, Cyprian Musiba hatumwi na Chama hicho na kama wanachakuzungumza yeye ndio mtoa kauli.

Polepole amesema kuwa Watanzania wanaotoa kauli kila pahala waendelee kutoa kauli maadam hawavunji sheria za nchi.

"Musiba hatumwi na Chama cha Mapinduzi na kama chama kinataka kutoa kauli mtoa kauli ni mimi hapa, lakini nataka nikwambie kuwa wapo Watanzania wanaotoa kauli kila pahala waendelee kutoa kauli maadam hawavunji sheria za nchi na wahamasisha waendelee kutoa kauli mbalimbali maadam hawavunji sheria za nchi hiyo ndio rai yangu," alisema Polepole.

Aidha Polepole amesema Chama hicho kinaongozwa na Katiba, Kanuni na Taratibu zilizowekwa, sio dhambi kiongozi yoyote kufanya ziara ila utaratibu wa ndani ya Chama ufuatwe
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad