Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameahidi kushughulikia jimbo lililokuwa na Tundu Lissu (Singida Mashariki) kwa upande wa Maji.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa Rada mbili (2) za kuongozea ndege za Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanajaro (KIA). Hafla inayofanyika katika Uwanja wa Ndege.
“Namheshimiwa nani yule aliyekuwa kwenye jimbo lililokuwa limetelekezwa la nani vile.. (Wananchi "La Lissu") ameshika huyu na ameingia na kazi kwasababu saa zingine kwenye majimbo kuna kosa wawakilishi. Kama ulivyosema Mheshimiwa Spika kwamba tushughulikie tatizo la maji katika jimbo lile…kama tulivyoshughulikia jimbo la Dar es Salaam…ninakuahidi kwamba serikali yangu itashughulikia," amesema Rais Magufuli.