Rais Magufuli amtaka Rais Mseven kuwa mkali kwa watendaji wake wa Mamlaka ya Mapato nchini Uganda (URA)

Rais Magufuli amemtaka Rais  Yoweri Museven wa Uganda kuwa mkali kwa watendaji wake ambao wanakwamisha kuanza kwa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini humo mpaka Tanga, Tanzania.

Magufuli ametoa mfano wakati alipoingia madarakani Novemba 5, 2015 alibadilisha makamishna wakuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) watano lengo ni kuongeza ufanisi katika mamlaka hiyo.

“Leo niwape siri, nilikuwa namuuliza Rais Museveni mbona unachelewesha hili bomba, kwa sababu ya kodi ya huko ambayo umekataa kuikubali ya Dola 600 wakati utakuwa unatengeneza Dola bilioni 800 jitolee hii kodi kidogo utengeneze ajira na utakuwa unapata fedha kwa muda mrefu watu wako wa TRA wasikucheleweshe, sisi tulitaka hilo bomba liitwe Kaguta Pipeline siku tunapozindua, hao wasikucheleweshe.

“Simfundishi mzee, lakini nilipoingia madarakani nimebadilisha makamishna watano kwa miaka mitatu na nusu, si suala la kujidai lakini ni baya. Nikamwambia wewe umeng’ang’ania huyo wa kwako wa nini huko, tunatakiwa twende mbele, katika biashara kuna kupata na kukosa unatakiwa utoe ili upate zaidi.

“Kwanini ucheleweshwe na watendaji, kaka naona umekuwa mpole kabla ya wakati ule ulipopigana ulikwa mkali sasa uongeze, ongeza ukali kwenye hili.

“Nimeona nilizungumze hili sitaki kuwa mnafiki, I wish (natamani) hawa watendaji wangehamia Tanzania na wa Tanzania waende Uganda nideal (nishughulike) nao kwa mwezi mmoja tu,” amesema Rais Magufuli.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad