Rais Magufuli Awaongezea Siku 7 Watuhumiwa wa Uhujumu Uchumi Kuomba Msamaha


Rais Magufuli ameongeza siku 7 zaidi kwa watuhumiwa wa rushwa na uhujumu uchumi kuomba msamaha baada ya DPP kuomba aongezewe siku tatu kutokana na wengine kushindwa kukamilisha taratibu za kisheria kwa wakati.

"Sikutegemea kama watuhumiwa 467 wa kesi za uhujumu chumi wangeandika barua wakiomba wasamehewe, najua DPP una barua nyingine zimekwama kwenye ofisi zako za Mikoa, na kama kweli wapo waliokwamishwa kwa sababu ya umbali, nimeongeza tena siku 7 iliusije ukaniomba tena"

"Natoa wito kwa Watanzania wenye tuhuma za uhujumu uchumi, wasiwe na wasiwasi kwamba ukishakiri basi kesho ndiyo ushahidi huo, siwezi nikafanya kazi ya kitoto namna hiyo, nimeshasema nimetoa msamaha ni msamaha kweli,hakuna msamaha wa majarbio au wa kumtega mtu, wasidanganywe"

"Katika siku 7 wapo ambao walizuiliwa na Maofisa wa Magereza wakitaka hongo kidogo kwamba unatuachaje hapa ndani,Kamishina wa Magereza upo hapa mkafuatilie waliomba msamaha kwa DPP msiwakwamishe, hizi Bilioni 107 zitatumika kufanya mambo mengi makubwa kwa ajili Taifa hili"

"Nakiri kwa kweli sikutegemea kama wangejitokeza 467 inawezekana hao waliochelewa wanaweza kufika hata 500, ila mfanye haraka ili mhakikishe hawa watu waliokiri wanasemehewa na wanatoka kwenda kuendeleza biashara zao ambazo zilikwama na musiwalazimishe watu kuomba msamaha"

"Huu msamaha sio wa uongo narudia tena, kuna Mawakili wanawadanganya ili waendelee kuwachomoa hela zenu, wasiwadanganye wanataka muendelee kukaa gerezani na mkikaa msimlaumu mtu"

"Nitoe tahadhari baada ya siku hizi wote watakaoshikwa na uhujumu uchumi, sheria ifuate mkondo wake, isije ikaonekana kesi za uhujumu uchumi hazipo au nimezifuta, watakaoshikwa leo au kesho waendelee na kesi zao, hizi siku saba ni kwa ambao wameandika barua zimekwama"
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad