Rais wa Afrika Kusini Amteua Aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu Tanzania Prof. Benno Ndulu Kuwa Mshauri Wake Wa Masuala ya Kiuchumi
0
September 28, 2019
Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amemteua Prof. Benno Ndulu kuwa miongoni mwa watu 18 wanaounda Baraza la kumshauri Rais huyo katika masuala ya uchumi litakaloanza kufanya kazi kuanzia Oktoba 01, 2019
Baraza hilo lililotangazwa jana na Rais Ramaphosa litakuwa na kazi kubwa ya kuhakikisha uhusiano mzuri na uthabiti katika utekelezaji wa sera ya uchumi na kuhakikisha kuwa Serikali inaweza kujibu mabadiliko ya hali ya uchumi
Baraza linajumuisha viongozi wa ndani na nje ya Afrika Kusini watakaotoa mawazo ya kiuchumi, wakimshauri Rais na Serikali kwa upana zaidi, kuwezesha maendeleo na utekelezaji wa sera za uchumi zinazochochea ukuaji wa umoja
Pamoja na Prof. Benno Ndulu, wengine ni Prof. Mzukisi Qobo, Prof. Dani Rodrik, Prof. Mariana Mazzucato, Mamello Matikinca-Ngwenya, Dkt. Renosi Mokate, Dkt. Kenneth Creamer, Prof. Alan Hirsch, Prof. Tania Ajam, Dkt. Grové Steyn, Wandile Sihlobo, Dkt. Liberty Mncube, Prof. Fiona Tregenna, Prof. Haroon Bhorat, Ayabonga Cawe, Prof. Vusi Gumede, Dkt. Thabi Leoka na Prof. Imraan Valodia
Prof. Benno Ndulu alikuwa Gavana wa Benki Kuu Tanzania tangu 2008 hadi 2018 baada ya Rais John Magufuli kumteua Profesa Florens Luoga kushika nafasi hiyo.
Tags