Rais wa Nigeria Kufanya ziara ya Kikazi Nchini Afrika Kusini



Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi nchini Afrika Kusini. Kwa mujibu wa ofisi ya rais ya Afrika Kusini ziara hiyo inatokana na vurugu za chuki dhidi ya wageni, ambazo zimesababisha mvutano baina ya mataifa hayo mawili.

Katika siku za hivi karibuni maeneo ya jiji la kibiashara la Afrika Kusini, Johannesburg, yalikumbwa na vurugu zilisosababisha mauwaji dhidi ya wageni, wengi wa walengwa wakiwa wafanyabiashara wa Nigeria na mali zao.

Vurugu hizo zilisababisha mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya makupuni ya Afrika Kusini nchini Nigeria na kufungwa kwa muda mfupi kwa ubalozi wa Afrika Kusini mjini Lagos.

Takribani watu 10 walipoteza maisha katika vurugu hizo na mamia ya maduka yaliharibiwa vibaya.

Taarifa ya ofisi ya rais ya Afrika Kusini imesema ziara ya Buhari ina lengo la kuimarisha uhusiano baina ya mataifa hayo mawili na kufanya jitihada ya pamoja katika kukabiliana na changamoto zinazowakabili watu na biashara kati ya Afrika Kusini na Nigeria.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad