Rais wa Zamani wa Ufaransa Afariki Dunia


RAIS wa zamani wa Ufaransa, Jacques Chirac, aliyeiongoza Ufaransa kati ya mwaka 1995 na 2007, ameaga dunia Alhamisi (26.09.2019) akiwa na umri wa miaka 86.

Mwanasiasa huyo mkongwe amekufa leo Septemba 26, 2019, asubuhi akiwa amezungukwa na watu wa familia yake.



Mkwe wake Frederic Salat-Baroux aliliambia shirika la habari la Ufaransa AFP. Hata hiyo hakueleza sababu ya kifo chake.

Chirac aliyefuata siasa za mrengo wa wastani zinazoengemea kulia, alihudumu kama meya wa jiji la Paris na aliwahi kuwa waziri mkuu mara mbili kabla kuwa rais mwaka 1995 hadi 2007. Hali yake ya afya ilidhoofika tangu alipopatwa na kiarusi mwaka 2005 alipokuwa madarakani.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad