RC Chalamila alivuruga jiji la Mbeya, ‘Hawa wamechokoza nyuki’


Mkuu wa Mkoa Mbeya, Albert Chalamila, amesema kuwa wananchi ambao walishambulia msafara wa Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Claudi Kitta wamechagua kuuawa, kwa kile alichokieleza wao walionyesha nia ya kumuua Mkuu huyo wa Wilaya.

RC Chalamila ametoa kauli hiyo katika kata ya Ghana, jijini Mbeya ikiwa siku chache baada ya Msafara wa Mkuu wa Wilaya ya Kyela kushambuliwa na wananchi wa Kijiji cha Mpunguti.

Amesema kuwa kwasababu walirusha mawe na walichagua kumuua Mkuu wa Wilaya (Kyela) na Kamati ya Ulinzi na Usalama nao wamechagua kuuawa.

“Nawaambieni ukweli hapa bado sijafungua kikosi kingine, tunasubiri watu waaanze tena ili tupige king’ora cha mwisho.” amesema Chalamila.

Hata hivyo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Jeromi Ngowi, alisema jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ili kuweza kuwabaini wale wote  waliohusika na kuvamia msafara wa Mkuu wa wilaya ya Kyela Claudi Kitta,  katika Kijiji cha Mpunguti wilayani humo.

Mbunge wa Mbeya mjini ‘Sugu’ afunga ndoa
RC Makonda awashangaa Chadema, ‘Akili ndogo haiwezi kujadili mambo makubwa’

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad