Usikivu wetu ni katika wimbo mpya wa Rich Mavoko ambao waitwa Babilon. Ni wazi tunamsikia Mavoko yule wa kabla ya Wcb lakini baada ya Wcb. (Uhalisia)
Na utulivu wake katika uimbaji ni wenye nogesho kuu la kuvutia katika kila kipande cha wimbo. Amekuwa ni makini mno, lakini daima “Umakini huleta utulivu”. (Hakika)
Rich hana haraka ya kuimba hana pupa hata mara moja. Lakini hapa katika jana yake ya muziki haikuwa njema bali pupa isiyo na maana. (Papara)
Na “Mwenye pupa hadiriki kula tamu” ndiyo maana ikawa kila wimbo ni anguko. Wajuzi walisema yakuwa “Alitoa nyingi kwa haraka ili kuonyesha yu bora. (Eeh)
Kimsingi hakupaswa kwa maana yeye ni bora tangia tangu na tangu. Isipokuwa mkwamo wake leo ni upana wa matangazo pekee. (Naam)
Hakuna cha ziada kama namna ya matangazo katika wimbo. Ni wazi wimbo huu ni mzuri na wenye utofauti katika soko kwenye usikivu mkuu. (Tungo)
Na daima ukipeleka bidhaa tofauti sokoni lazima iwe bora lakini ujazo wa matangazo utafanya iwe ni katika uuzaji kamili. (Faida)
Mavoko apunuke katika matangazo kuanzia ngazi ya mtandao mpaka kwenye vyombo vya habari kawaida. (Ukamili)
Isiwe ishio la Clouds Fm pekee, bali kila chombo na wimbile kwa upana wa kila mosi. Akiamka kifikra na uongozi imara hakika wimbo huu ni ngazi yake ya kurudi katika nafasi yake. (Ujuzi)
Tizneez