Sabaya Ataja Sababu ya Kuwakamata Viongozi CHADEMA


Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya, amezitaja sababu zilizopelekea yeye kuagiza viongozi wanne wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wakamatwe ni pamoja na wao kufika katika Shule ya Sekondari Rundugai kufanya siasa, eneo ambalo si la kwao bila kutoa taarifa kwa Mkurugenzi w

Akizungumza leo Septemba 20 na EATV&EA Radio Digital, Sabaya amesema kuwa viongozi hao wamekuwa na utaratibu huo wa kwenda katika eneo hilo mara kwa mara kwa madai ya kwamba wanaenda kutoa msaada badala yake wanaishia kupiga picha na wanafunzi na kwenda kujinadi wametoa msaada.

''Ni kweli nimetoa amri ili wakamatwe kwasababu wamekuwa wakifanya kama mazoea na hii ni mara ya tatu na mwanzo nilikuwa nikiwavumilia tu, kwanini wasiende kufanya siasa zao huko Ngorongoro, wanakuja kuwalaghai laghai wanafunzi na kuishia kupiga nao picha'', amesema Sabaya. 

Sabaya ameongeza kuwa viongozi hao walifika Shuleni hapo wakitaka kuzungumza na wanafunzi ili kujua mahitaji yao kwa kutaka kuwasaidia, kitendo ambacho anakiona ni cha kisiasa.

Mbali na Mbunge Lucy Owenya, viongozi wengine waliokamatwa ni pamoja na mwenyekiti wa Halmashauri ya Hai Helga Mchomvu, Katibu wa Mbunge wa Hai Irene Lema na Diwani wa Machame kaskazini Clement Kwayu na wamepelekwa katika kituo cha polisi cha Bomang'ombe.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad