Sakata Kulipia Maiti Latikisa Bunge, Waziri Asimama


SERIKALI imetakiwa kupitisha utaratibu ambao hautawabana watu kuchukua miili ya ndugu zao waliofariki wakati wa matibabu katika hospitali zake.

Wito huo umetolewa bungeni leo, Septemba 6, 2019, na wabunge wa Viti Maalum, Susan Lyimo (Chadema)  na Faida Bakari (CCM) waliotaka kukomeshwa kwa utaratibu huo ambao huongeza simanzi kwa wafiwa.

“Je ni lini serikali itaacha kutoza gharama miili ya marehemu wanaofia hospitali na kuhifadhiwa katika vyumba vya  maiti (mochwari) ili kupunguza simanzi kwa wafiwa?” aliuliza Lyimo kuhusu suala hilo ambalo liliungwa mkono pia na Bakari.

Akijibu hoja hiyo, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amesema serikali haizuii ndugu wa marehemu kuchukua miili ya wapendwa wao kutokana na gharama za kuhifadhi miili hiyo, bali inafanya hivyo ili ndugu wa marehemu wamalizie madeni ya matibabu wakati akiwa mgonjwa.

Aidha, akielezea zaidi, waziri huyo alisema serikali imeweka utaratibu wa msamaha kwa watu wasio na uwezo wa kulipia madeni hayo na kuruhusiwa kuchukua miili ya ndugu zao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad