Samatta Kupewa Mtaa Kibiti

BABA Mzazi wa Mshambuliaji wa KR Genk ya nchini Ubelgiji, Mbwana Samatta, Mzee Ally Samatta ametuma maombi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti kumpatia mtaa mtoto wake huyo kutokana na historia aliyoiweka katika soka la Tanzania kwa kuwa eneo hilo ndio chimbuko lake.



Samatta ambaye anakipiga Genk ameweka rekodi kadhaa katika soka la Tanzania ikiwa ni pamoja na kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya, Mchezaji Bora Afrika akiwa na TP Mazembe pamoja na kucheza ligi ya Ubelgiji historia ambayo haijawekwa na mchezaji mwingine hapa nchini.


Akizungumza na Spoti Xtra Mzee Samatta alisema kuwa; “Baada ya mheshimiwa Makonda kumpa Samatta mtaa hapa Dar, nimeonelea ni vyema kupeleka maombi kwa wakuu wa Wilaya ya Kibiti ili kuweza kumpa heshima na kujua chimbuko lake ni wapi, Samatta ni Mdengeleko halisi, mimi baba yake nimetokea huko Kibiti hivyo ni vyema kuweka ukumbusho.”



“Ingekuwa fahari kuona Mndengeleko kutoka Rufiji ndio amefanikiwa kuweka rekodi katika historia ya soka la nchi hii pia kuwafahamisha watu kujua Samatta ametokea wapi.



“Tayari nimeshatuma maombi hayo na yanafanyiwa kazi iwapo watakubaliana na ombi langu basi wakati wowote anaweza kupewa mtaa,” alisema Mzee Samatta.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad