Samatta, Watanzania tuna ndoto za kitaifa kwako kaka
0
September 03, 2019
Tanzania ni ya Mbwana Samatta, Tanzania ni ya Mbagala na Tanzania ni mtu mmoja linapokuja suala la soka kwenye nyanja za kimataifa. Mbwana Samatta ndiye anayebeba ndoto za nchi hii katika kuwa mwanya utakaoruhusu Watanzania wengine kunufaika na kufika mbali kupitia soka.
Ni ndugu yetu ambaye miguu yake tangu akiwa na Simba mpaka TP Mazembe, ilijenga urafiki wa karibu na nyavu na uhusiano wao ukawa imara kuliko marafiki wengi alionao mpaka ikampatia VISA ya Ubelgiji na sasa yupo na klabu ya KRC Genk.
Mchezaji bora wa Afrika wa wachezaji wa ndani mpaka mchezaji bora mwenye asili ya Afrika anayecheza ligi ya Ubelgiji yote yaliandikwa na yote yakawa sehemu ya ndoto ya Taifa na ndoto zake binafsi. Hata hivyo inawezekana kabisa yote haya kwa pamoja yalikuwa aina ya mapishi huku chakula pekee ambacho Watanzania walitamani kukila kutoka kwake ikawa ni ligi tano kubwa. Chakula ambacho wanaweza kukipata kwa urahisi kutoka sebuleni kwao kupitia runinga, chakula ambacho kinafuatiliwa duniani kote, yaani Ligi Kuu England, Hispania, Ujerumani, Ufaransa na Italia.
Kila mtu alitamani kuona Samatta akikimbizana kwenye mbio za magoli na Aubameyang, Salah na Mane, acheze mechi na Ronaldo na kila mmoja afunge au afunge goli kwenye mchezo ambao Messi hatofunga kabisa na pia afunge goli ambalo lingeweza kumkera Neymar pale Ufaransa. Haya ni maisha ya ndoto, maisha ambayo Watanzania tumeungana kwa maombi tukihitaji baraka juu ya Mbwana ili afike huku.
Huku yote haya yakionekana kutokuwezekana walau kwa msimu huu, hata baada ya msimu uliopita kumfunga Loris Karius, kipa wa zamani wa Liverpool, kuna nafasi kubwa zaidi kwa Mbwana Samatta, fursa bora zaidi kama atakuwa na kiwango cha msimu uliopita. Bahati nzuri tayari kaanza msimu kwa kasi ile, na sasa mwaka huu kikombe chenye dhahabu kipo mbele yake, kinaitwa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.
Mbwana Samatta atakuwa anacheza moja ya michezo itakayotizamwa zaidi duniani, dhidi ya klabu bora na maarufu ulimwenguni hususani kwenye mashindano ya Ulaya.
Mchezo utakaohusisha klabu yenye mchezaji bora wa Ulaya, Virgil van Dijk, mfungaji bora mara mbili mfululizo Ligi Kuu nchini England, Mohamed Salah na kwa ujumla bingwa mtetezi wa michuano hii na klabu inayoaminika kuwa na washabiki bora duniani, Liverpool FC.
Tumeukosa usajili wa Ulaya sasa umefika wakati wa kuutumia usiku wa Ulaya. Umefika wakati wa Samatta kupanda thamani zaidi. Usiku wa kumfanya Florentino Perez afute miwani yake, usiku ambao utasababisha kelele za kitaifa kwa kila goli atakalofunga na usiku ambao utaweka rekodi ya Mtanzania kucheza na kufunga goli kwenye Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.
Inaweza kutuchukua muda mrefu kuona kijana mwingine kwenye mashindano haya lakini kila “touch” ya Samatta kwenye eneo la kumi na nane itaongeza skauti mmoja au zaidi nchini na kila goli litaongeza nafasi kwenye upenyo mdogo wa Watanzania kuendelea kuonekana kwenye mataifa yaliyoendelea kisoka. Tunausubiri usiku wa Ulaya, tunasubiri ongezeko la thamani ya Euro kwenye thamani iliyopo ya Mbwana Samatta.
Tunausubiri usiku ambao utasababisha kwenye kitabu chake ambacho kitakuja kuandikwa, huu mwaka utaelezewa vyema, unaweza kuwa na stori nzuri kuliko zile za Simao Sabrosa, Thierry Henry au hata Arsene Wenger kuhusiana na Anfield. Hii itabeba mada iliyobebwa na uhalisia wa mitaa ya Mbagala, ngoma za Lubumbashi pale Mazembe mpaka ndoto ya kelele za Anfield. Ndoto ya kitaifa imechelewa lakini haijakoma, tunaiona ikija kwa kasi tofauti. Tumevuta mito yetu, na harufu yake inatupa usingizi mzito, usingizi murua, usingizi wenye ndoto kuu, ndoto ya Mbwana Samatta. Tulitamani angekuwa anaishi London, Barcelona au Turin lakini sasa atakuwa anatoka Ubelgiji na kutua huku na sisi tutamfuata kwa pamoja, tutakuwa mbele ya luninga zetu na hatutokoma.
Tupo na vikokotoleo vyetu, tutahesabu idadi ya mipira atakayogusa, krosi atakazopiga na magoli atakayofunga. Tutamlinganisha na Mohammed Salah na Sadio Mane na tutakuwa tunajiandaa na ile tuzo ya mchezaji wa Afrika pia. Tumejipanga kwa mengi, tumejipanga kwa utalii kutumia jina lako na tumejipanga kushuhudia ukipita ukuta wa chuma uliosimikwa na Virgil van Djik. Hizi zote ni ndoto lakini tunaamini utazitimiza.
Wakati kukiwa hakuna mfumo bora na imara uliowekwa muda mrefu, pia hawana namna nzuri ya kudumu na makocha. Hawana mpangilio mzuri wa kuchagua makocha na pia hawana njia bora za usajili ambazo zinaweza kuendana na makocha wanaowahitaji. Na hapa ndipo picha kubwa ya Ndayiragije inapokuja kwenye akili yangu.
Hapo ndipo ninaona picha mbili za shilingi yake, hususani namna ambavyo Azam ilicheza dhidi ya Simba iliyolala mlango wazi kwenye Ngao ya Jamii.
Ndayiragije anakutana na presha mbili, mosi ni kuwa hajawahi kuwa katika presha hii na pili ni kuwa alikuwa bosi anayesikilizwa kwenye klabu alizotoka jambo ambalo halitakuwepo kwa sasa.
Ataishi katika misingi ya kutazamwa anafanya nini na kipi kinakuja mbele yake. Bahati mbaya zaidi kuna kazi inayotamanisha inaitwa Taifa Stars, huku nako akipatia kunaweza kuleta presha upande wa pili.
Anaishi maisha ya presha kwa sasa, kuhakikisha anatimiza majukumu yake kwa ufanisi.
Natamani awe wa kwanza kuleta mabadiliko, awe wa kwanza kutulia na awe wa kwanza kusaidia upatikanaji wa wachezaji bora na watakaotulia kwenye klabu muda mrefu.
Kubwa zaidi ni yeye kuweza kusaidia tukaliona lile giza jipya litalokuwa chanzo cha mwanga wa maana, mwanga wa ufalme wa Azam.
Bado tunahitaji hili, lakini kwanza awe makini kwa sababu wanamtazama tu, wapo wanaomtafutia kutokana na presha aliyonayo huku TFF nao ikiandaa mkataba kisiri kama atapatia katika kuongoza Taifa Stars.
Ni macho manne kwa Ndayiragije mawili akiyaelekeza kwa Azam na Stars na mengine yakisubiri akosee.
Tags