Samuel Eto’o Astaafu Soka

NYOTA wa zamani wa klabu za Barcelona, Inter Milan na Chelsea, mshambuliaji Samuel Eto’o, ametangaza kustaafu soka akiwa na uri wa miaka 38.

Mchezaji huyo wa  Cameroon aliyeanza kuandika jina lake katika soka ya ulimwengu mwaka 1997, amefunga mabao 350 katika klabu alizochezea na aliwahi kuwa Mchezaji Bora wa Mwaka wa Afrika mara nne.

Akiwaaga mashabiki zake, ame-posti ujumbe kwenye mtandao wa  Instagram, usemao:

“Mwisho wa yote.  Nalekea kwenye majukumu mengie.  Asanteni, nawapenda sana.”

“The end. Towards a new challenge. Thank you all, big love.”


Nyota huyo alipitia pia klabu mbalimbali akimalizia soka lake katika klabu za Anzhi Makhachkala, Chelsea, Everton, Sampdoria, Antalyaspor, Konyaspor na hatimaye  Qatar SC.

Alikuwa mchezaji mdogo zaidi katika fainali za Kombe la Dunia mwaka 1998 alipokuwa na umri wa miaka 17 tu katika kikosi cha Cameroon ambapo baadaye alitunukiwa medali ya dhahabu katika Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2000 na katika fainali za Kombe la Afrika mwaka  2000 na 2002.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad