Senga na Pembe wamvaa Pierre Liquid


Wachekeshaji wa muda mrefu nchini Tanzania, Pembe na Senga wamefunguka kuhusu urafik wao, kugombanana Pierre Liquid pamoja na jinsi walivyoingia katika sanaa ya uchekeshaji.


Wawili hao ni marafiki wa muda mrefu lakini licha ya muda mrefu wa urafiki wao, wamekiri kuwa huwa wanagombana na kuwekana sawa pale ambapo wanakoseana.

“Niliwahi kumpiga huyu hadi aliamuliwa na mkewe, kugombana kwetu ni lazima na msipogombana kupatana hakuna ila mkigombana mtajuana kama mwenzangu kitu hichi anapenda au hapendi ndiyo maana tupo pamoja muda mrefu na kugombana kwetu ni masharti”, ameeleza Senga.

Wakizungumzia kuhusu Pierre Liquid kuingia katika sanaa ya uchekeshaji na kuteka Watanzania kwa kipindi kifupi, Senga na Pembe wamesema,

“Wataalamu binafsi wanasema Pierre Liquid ni mchekeshaji lakini wataalamu wa viwango wanasema Pierre ni mlevi, sanaa ni sanaa na ulevi ni ulevi ila Pierre anaweza akawa msanii kama ataingia darasani lakini vitendo anavyofanya anawakilisha mlevi alivyo” wameeleza Senga na Pembe wakiwa wanachangia mada.

Aidha wameendelea kusema kuwa Pierre ni mlevi halisia na anachofanya sio sanaa na hatakiwi kupewa sifa ya msanii.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad