Serikali ya Tanzania yalaani vurugu zinazoendelea Afrika Kusini


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamaganda Kabudi, amesema vuguvugu linaloendelea nchini Afrika ya Kusini, hatuwezi kulielewa bila kuelewa historia ya nchi hiyo kwa sababu ni kwa kipindi kirefu wananchi wake walinyimwa haki zao chini ya ubaguzi wa rangi.

Waziri Kabudi ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa habari katika hafla maalumu ya kuwaaga vijana 100, wanaokwenda nchini Israel kwa ajili ya mafunzo ya kilimo kwa vitendo  na kusema, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeunga mkono kauli ya kulaani vitendo hivyo iliyotolewa na Rais wa nchi hiyo Cyrill Ramaphosa.

”Serikali ya Tanzania inaunga mkono kauli iliyotolewa na Rais wa Afrika ya Kusini Cyrill Ramaphosa  ya kulaani vikali na kukemea vitendo hivyo na serikali inaendelea kuwa na mawasiliano ya karibu na Serikali ya Afrika Kusini kwani vuguvugu hizo zimetia doa nchi hiyo,” amesema Profesa Kabudi.

Hadi sasa vimeripotiwa vifo vya watu takribani watano, huku wengine wakijeruhiwa pamoja na kuharibiwa mali zao, vurugu ambazo zinafanywa na baadhi ya vijana wazawa kwa madai ya kwamba Waafrika kutoka nchi zingine wanawachukulia ajira na kazi zao.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mzee chonde ongea na mawaziri wa mambo ya nje wenzako wa africa, muipe lesson Africa ya kusini. Kama wameweza kujifunza roho mbaya toka kwa counterparts wao makaburu kupitia msimu wa ubaguzi wa rangi, basi wanao uwezo wa kujifunza utu wema endapo watapewa lessons. Napendekeza lessons nzuri ni kuwawekea vikwazo mpaka watakapokiri wanetubu. Na hii isiwe kwa Africa ya kusini pekee. Bali hata kwa wa africa walioodoka enzi za biashara ya utumwa kokote walipo duniani. Huko waliko identity yao inaanza na waafrica wamarekani. Maana wanawaona wao ni waafrica. Sisi huku Africa badala yake tunawaona ni wamarekani. Inasikitiasha indeed, kumbe hatujatubu kwa vitendo dhambi ya kuwauza mababu zetu kupitia biashara ya utumwa. Wale wa maerekani wanajiona hawana pa kukimbilia kwa sababu hakuna aliyewahi (Sina hakika) kuwaita nyumbani kama Nigeria inavyofanya sasa kwa wanaigeria wa sauzi.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad