SERIKALI imesema itaendelea kuboresha Miundombinu ya huduma mbalimbali Muhimu magerezani ikiwa ni pamoja na ujenzi wa zahanati Katika Magereza yaliyo na changamoto hiyo.
Hayo yamesemwa leo Sept.10,2019 Bungeni jijini Dodoma na naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi,Mhandisi Hamad Masauni wakati akijibu swali la Mbunge wa Kilombero Mhe.Peter Ambrose Lijualikali aliyehoji Kumekuwepo na changamoto ya kutokuwa na zahanati baadhi ya magereza hali ambayo hulazimu wafungwa kupelekwa kupata huduma za afya nje na Magereza ,je,serikali ina mpango gani wa kujenga zahanati katika magereza yote nchini.
Katika majibu yake Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mhandisi Hamad Masauni amesema katika maeneo yaliyo na upungufu wa nguvu kazi ya madaktari pamoja na Zahanati serikali inaendelea kuwa na mkakati wa kupunguza suala hilo pindi fedha zinapopatikana.
Katika Mkutano wa 16 wa bunge na kikao cha 6 ,hati ya Waziri wa Maliasili na Utalii imewasilishwa kuhusu azimio la kuridhia mapendekezo ya ubadilishaji wa hadhi sehemu ya eneo la pori la Kigosi kuwa Hifadhi ya Taifa ya Kigosi pamoja na azimio la kuridhia mapendekezo ya ubadilishaji wa Hadhi Sehemu ya eneo la pori la akiba Ugalla kuwa Hifadhi ya Taifa ya Mto Ugalla.