Shamsa Ford Afunguka Kuhusu Mapenzi..Awapa Soma Kinadada Wanaongia Mapenzini Jumla Jumla


"Mapenzi yana nafasi kubwa sana kwenye maisha yetu na mbaya zaidi hayakwepeki.Kuna waliopoteza uhai kwasababu ya mapenzi na wengine wakakata tamaa ya maisha kabisaa kwasababu ya mapenzi.

Mapenzi yanaweza yakakuharibia maisha bila kutegemea coz wengi wakipenda huwa hata akili ya kujishughulisha na maisha wanasahau.Hakuna ambae hajawahi kuumia au kulia kwa ajili ya mapenzi.Mapenzi yanaweza yakaharibu dira ya maisha yako na ukaonekana kituko kwenye jamii bila kupenda..

Wanaopitia changamoto kubwa kwenye mapenzi ni wanawake. Mwanamke akipenda huwa anaingia na miguu miwili na hata kama kuna mashimo atayaziba tu ilimradi tu airidhishe nafsi yake.

Kuna muda mwanamke anaumizwa mpaka anajiona yeye si wa thamani wakati siyo kweli.Mwanamke unayelia futa machozi na ujue kuwa wewe ni wa THAMANI sana ndomaana ukaumbwa"
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad