Shilole Ampa Somo la ndoa Alikiba "Ndoa Inaongozwa na Upendo Ndio mana Mimi na Mume Wangu Uchebe Tunadumu"


WAKATI msanii Ally Saleh Kiba ‘AliKiba’ ndoa yake ikiwa inapumulia mashine kutokana na migogoro, mrembo kutoka Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shishi’ amempa somo la ndoa msanii huyo kwa kumwambia ndoa inaongozwa na upendo.  Shishi alisema, kutokana na upendo wa dhati walionao yeye na mumewe Uchebe pamoja na hofu ya Mungu waliyonayo ndiyo silaha kubwa ya wao kudumu hivyo kama Kiba na mkewe Amina Khalef hawana hivyo vitu wanapaswa kuvitafuta kwanza.

“Hii ndiyo silaha yangu mimi na mume wangu, hakuna uchawi wala ndumba. Tuna muda mrefu sasa na ndoa yetu ipo imara na hakuna mtu wa kututenganisha,” alisema Shishi au Shilole anayetamba na Wimbo wa Nikagongee Remix aliofanya na Buddest 47.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad