Spika Pelosi Aanzisha Uchunguzi Rasmi Kuhusu Madai ya Ukraine Yanayomuhusisha Trump

Chama cha Marekani cha Democrats kimeanzisha uchunguzi rasmi dhidi ya rais wa nchi hiyo Donald Trump kuhusiana na madai kwamba alitaka usaidizi kutoka kwa taifa la kigeni ili kumuangamiza hasimu wake wa kisiasa.

Spika wa bunge la congress kutoka chama cha Democrat Nancy Pelosi amesema kuwa rais "lazima awajibike ".

Bwana Trump anakanusha madai hayo na amezitaja juhudi za kumtuhumu kama " hila chafu'' dhidi yake .

Huku kukiwa na uungaji mkono mkubwa kutoka kwa wafuasia wa Democrats juu ya uchunguzi huo unaoweza kumuondoa mamlakani , ikiwa utaendelea huenda usipitishwe na baraza la seneti - linalodhibitiwa na wabunge wa chama cha Trump cha Republican.

Mzozo huo ulichochewa na ripoti za jasusi aliyefichua malalamiko kuhusu simu ambazo rais Trump alimpigia mwenzake wa Ukrain rais Volodymyr Zelensky.

Awali Spika Nancy Pelosi alikataa kuanzishwa kwa uchunguzi dhidi ya rais
Kuhusu ni nini hasa alichosema limesalia kuwa lisilo wazi , lakini Democrats wanamshutumu Bwana Trump kutishia kusitisha msaada wa kijeshi kuishinikiza Ukraine kuchunguza madai ya rushwa dhidi ya makamu wa rais wa zamani Joe Biden na mtoto wake wa kiume Hunter.

Bwana Trump amekiri kuwa alimzungumzia Joe Biden na Bwana Zelensky lakini akasema alkuwa tu akijaribu kuitaka Ulaya iingilie kati kutoa msaada kwa kuitishia kusitisha msaada wa kijeshi.

Bi Pelosi amesema nini ?

Bi Pelosi alisema kwua Bwana Trump amefanya kosa la "ukiukaji wa sheria ", na kuyataja matendo yake kama "uvunjaji wa wajibu wake wa kikatiba''.

"Wiki hii rais Trump alikiri kumuomba rais wa Ukraine kuchukua hatua ambazo zitamnufaisha kisiasa ," alisema, na kuongeza kuwa : "Rais lazima awajibishwe."

Kama Spika wa bunge, Bi Pelosi ni afisa wa ngazi ya juu zaidi wa Democrat. Bi Pelosi awali amekuwa akipinga miito ya kutaka amuondoe madarakani rais wa Republican akidai juhudi za aina hiyo zinaweza kuimarisha uungaji mkono kwa Trump.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad