"Tanzania ina matajiri na wanaotoa" - Makonda

 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema kuwa pesa ambazo huwa anaonekana akizigawa ni pesa ambazo anazipata kwa wadau na marafiki zake wa karibu ambao wako tayari kumuunga mkono katika masuala ya maendeleo.

Makonda ameyabainisha hayo leo Septemba 18, alipokuwa akizungumza mbele ya Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, walipokuwa wametembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ili kujionea utendaji kazi wa Taasisi hiyo na kupokea taarifa ya watoto ambao wamekwishapatiwa matibabu, kutokana na utaratibu wake aliouweka wa kusaidia watoto 10 kila mwezi.

''Sasa hivi Mh Waziri kuna watu wanauliza hivi Makonda anatoaga wapi hela, yaani yeye kila kitu ni yeye tena zile milioni kumi za Kaseja zimepigiwa kelele kweli,  jamani nchi hii ni tajiri na watu wa nchi hii ni matajiri, wanachohitaji ni mtu mwaminifu na mwadilifu anayeomba pesa kwa matumizi sahihi na watu hao watatoa pesa'', amesema Makonda.

Aidha Makonda yupo katika mchakato wa kuunda kamati maalumu ya kufunga mwaka, yenye mlengo wa kukusanya kiasi cha Shilingi Bilioni 1, kutoka katika makampuni mbalimbali, fedha zitakazosaidia kuokoa maisha ya watoto wenye matatizo ya moyo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad