Tanzania Yapanda Viwango vya FIFA, Hizi Hapa timu 10 zinazoongoza Afrika

Tanzania imepanda kwa nafasi mbili katika viwango vya soka duniani kwa mwezi Septemba vilivyotolewa leo na FIFA ikitoka nafasi ya 137 hadi nafasi ya 135.

Kwa mujibu wa viwango hivyo, Tanzania inakamata nafasi ya nne kati ya nchi tano za Afrika Mashariki, ikiipiku Burundi pekee ambayo imepanda kwa nafasi nne kutoka nafasi ya 148 hadi 144.

Uganda ndiye kinara wa Afrika Mashariki ikiwa imesalia kwenye nafasi yake ya 80 ikifuatiwa Kenya ambayo pia imesalia kwenye nafasi yake ya 107 na Rwanda iko nafasi ya 130 ikiwa imepanda kwa nafasi tatu.

Somalia baada ya kuichapa Zimbabwe kwenye mchezo wa kwanza wa kufuzu Kombe la Dunia, imepanda kwa nafasi tatu kutoka nafasi ya 202 hadi ya 199, huku Zimbabwe ikishuka kwa nafasi sita hadi nafasi ya 118 juu ya Kosovo waliopanda kwa nafasi moja hadi nafasi ya 119.

Kwa upande wa Sudan ambao watakutana na Tanzania kwenye mchezo wa kuwania kufuzu CHAN, wao wanakamata nafasi ya 128 wakiwa wamepanda kwa nafasi moja na wakiwa juu ya Tanzania kwa nafasi saba.

Namba moja duniani imeendelea kukamatwa na Ubelgiji, ikifuatiwa na Ufaransa, Brazil, England, Ureno, Uruguay, Hispania, Croatia, Colombia, Argentina, Uswizi, Mexico, Uholanzi, Denmark, Italia, Ujerumani, Chile, Sweden, Peru na Senegal ambayo imeendelea kusalia kwenye nafasi yake ya 20.

Afrika inaongozwa na
1. Senegal – 20.
2. Tunisia – 29.
3. Nigeria – 34.
4. Algeria – 38.
5. Morocco – 39.
6. Egypt – 49.
7. Ghana – 51.
8. Cameroon – 53.
9. Congo DR – 55.
10. Ivory Coast – 65.
11. Mali – 57.
12. Guinea -74.
13. Cape Verde – 78.
14. Uganda – 80.
15. Zambia 81.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad