Tanzia: Winga Wao Wa Zamani Timu ya Simba Afariki Dunia


Winga wa zamani wa Simba SC, wetu wa kushoto katika miaka ya sabini, Abbas Dilunga, amefariki jana na anatarajiwa kuzikwa leo kwao Kisarawe mkoa Pwani.

Dilunga alikuwepo kwenye kikosi kilichoweka historia pekee nchini mwaka 1974 kwa kufika nusu fainali ya klabu bingwa Afrika na pia alicheza mechi zote za kikosi kilichotwaa kwa mara ya kwanza ubingwa wa Afrika Mashariki na ya kati mwaka huo.

Taarifa zaidi juu ya msiba huo mkubwa kwetu tutaendelea kuwajuza katika mitandao yetu ya klabu.

Imetolewa na Haji S Manara, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba Sports Club.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad