Tenga na Washtakiwa Wengine Watano wa Uhujumu Uchumi Wamwandikia Barua DPP Kuomba Kukiri Makosa Yao


Washtakiwa watano wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi akiwemo wakili, Dk Ringo Tenga wamemwandikia barua Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP) kuomba kukiri makosa yao.

Wakili wa washtakiwa hao, Byrson Shayo ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Ijumaa Septemba 27, 2019 wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Dk Tenga ambaye ni mkurugenzi na mwanasheria wa kampuni ya mawasiliano ya Six Telecoms Limited na wenzake, wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 73/2019.

Washtakiwa hao  wanakabiliwa na mashtaka sita, likiwemo la kutakatisha fedha na kuisababishia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) hasara ya Dola za Marekani 3,748,751.

Mbali na Dk Tenga, washtakiwa wengine ni Hafidhi Shamte au Rashidi Shamte ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Mfanyabiashara na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Peter Noni, Mkuu wa fedha wa kampuni hiyo Noel Chacha na Kampuni ya Six Telecoms.

Wakili Shayo amedai  mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa wamejadiliana na wateja wao na baada ya majadiliano hayo wameamua kumuandikia DPP barua kwa kuzingatia maagizo ya Rais John Magufuli aliyoyatoa Septemba 22,  2019.

Amesema kutokana na uamuzi huo, wanaiomba mahakama kutoa ahirisho la siku 14 kuanzia leo ili waweze kupata  majibu ya barua hiyo.

Hakimu Simba baada ya kusikiliza maelezo hayo, ameahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 11, 2019 itakapotajwa na washtakiwa wamerudishwa rumande

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Chonde Chonde Hii ina Ukakasi.
    Msitumie jina la Mh. Raisi.
    Pesa kuruddishwa yote kwa wakati usiozidi siku 89. Ikiwemo zuio la kuusafiri nje ya mipaka ya TZ.

    DPP liangalie vizuri hili na Mh Raisi hakutoa Agizo ila ametoa RAI.

    Nia naLenngo ni kutaka Pesa zetu zirudi na hawa Wahujumu wawweze kurudi ktk Familia zao ili washiriki kulijenga Taifa kwa kufanya kazi Halali na kipato Halali.

    Wapotoshaji ..Msipotoshe.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad