Tunaishukuru Mahakama ya Afrika Kusini kwa kutenda haki - Dk. Ndumbaro

Mahakama Kuu ya Gauteng baada ya kuamuru kuachiwa kwa ndege ya Serikali ya Tanzania inayosimamiwa na Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) iliyokuwa imezuiwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo, Afrika Kusini tangu Agosti 24, 2019. Hatimaye Serikali yaishukuru Mahakama.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk Damas Ndumbaro amesema nchini humo kuwa, Mahakama hiyo imekubali hoja zote za mawakili wa Tanzania hivyo Serikali imeshinda kesi na ndege imeruhusiwa kuondolewa uwanjani hapo.

"Kwa hiyo sisi tunaishukuru sana Mahakama ya Afrika Kusini kwa kutenda haki lakini tunawashukuru zaidi Watanzania ambao wameunga mkono juhudi zetu za kuinasua ndege hii kutoka huku Afrika Kusini," amesema Dk. Ndumbaro.

Kwa mujibu wa Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Mahakama hiyo pia imeamuru mlalamikaji alipe gharama za kesi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad