Uchaguzi Israel :Vyama vya Kiarabu vyamuunga Mkono Gantz hasimu wa Netanyahu


Wabunge Waarabu nchini Israeli wamependekeza kuwa mkuu wa majeshi wa zamani Israeli Benny Gantz ndiye anayepaswa kuwa waziri mkuu wa Israeli.

Katika uchaguzi uliopita kiongozi wa Israeli Benjamin Netanyahu alikuwa bega kwa bega na Bwana Gantz, na wawili hao sasa wanawania kuunda serikali ya mseto.

Miongoni mwa vyama vilivyo katika orodha ya vile vitakavyounda serikali ya mseto ni pamoja na Muungano wa vyama vya waarabu ambavyo vilipata nafasi ya tatu vinavyosema vinataka kumuondoa mamlakani.


Picha: 'Sekunde kadhaa kabla ya ajali ya ndege'
Hii ni mara ya kwanza tangu mwaka 1992 kwa kikundi cha wanasiasa wa kiarabu nchini Israeli kumuidhinisha waziri mkuu

Huu ulikuwa ni uchaguzi mkuu wa pili wa mwaka wa Israeli . Baada ya uchaguzi wa kwanza , mwezi April , mazungumzo ya muungano yalivunjika kna uchaguzi ukaitishwa.

Akikabiliwa na mkwamo mwingine wa kisiasa , rais Israel Reuven Rivlin amependekeza kuwepo kwa serikali mpya itakayojumuisha miungano ya yote ule wa Blue wa Gantz na ule wa White pamoja na chama cha wazri mkuu Bwana Netanyahu cha Likud.

Bwana Rivlin amekwishasema kuwa atafanya kila liwezekanalo kuepuka uchaguzi mkuu wa tatu nchini Israeli mwaka huu .

Aymen Odeh, kiongozi wa mungano , amemuambia Rivlin kwamba kipaumbele cha muungano wao ni kumzuwia Bwana Netanyahu kuongoza kwa muhula mwingine.

Muungano huo wa vyama vya kiarabu una viti 13 bungeni . Bwana Gantz aliidhinishwa na wabunge wote 13 , lakini bado atahitaji viti 61 vinavyohitajika kupata wingiwa viti katika bunge lenye viti 120.

Huu ni mchakato muhimu wa mamlaka ya kisiasa kwa raia wa Palestina ndani ya Israel

Rais Rivlin anashauriana na viongozi wa chama kuhusu ni nani ambaye atamuomba kuongoza nchi baada ya matokeo ya uchaguzi wa wiki iliyopita ambao hayakutoa matokeo kamili . Vyaka vya kiarabu vimeonyesha nguvu kwa kuwa namba tatu kwa idadi ya viti vya bunge.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad