Ujumbe wa Godbless Lema kwa Sugu baada ya kufunga ndoa



Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amemwandika ujumbe mrefu Mbunge mwezake kutoka chama kimoja (CHADEMA) Joseph Mbilinyi 'Sugu' wa Mbeya Mjini baada ya kufunga ndoa hapo.

Chini ni kile alichoandika Lema

Kamanda Sugu umefunga ndoa takatifu na Mkeo Happy, neno la Mungu linasema "Apataye Mke apata kitu chema naye atapata kibali mbele za Mungu" kwa hiyo sasa mnacho kibali wewe na mke wako mbele za Mungu

Maisha ya ndoa ni maisha ya baraka sana na mafanikio, unapaswa kumpenda mke wako kwa dhati kabisa, kwani imeandikwa "enyi waume wapendeni wake zenu kama Kristo alivyo lipenda Kanisa hata akautoa uhai wake kwa ajili yenu

Shemeji Happy unapaswa kujua na kutambua kuwa silaha ya ndoa yako ni unyenyekevu kwani imeandikwa enyi wake watiini waume zenu, utii ni nguvu kubwa kwa mwanamke kulinda na kutunza ndoa bora.(Humility Is Not Slavery)

Wanawake walio wengi wanafikiri kuwa utii ni utumwa na hii imekuwa sababu kubwa ya ndoa nyingi kuyumba.Unyenyekevu na utii katika ndoa ni ibada na mwanamke akiishi kwa ibada ya aina hii basi ndoa itakuwa salama na bora.

Kamanda Sugu,mapenzi ya kweli ktk ndoa yana jengwa kwa kumcha Mungu,sababu ya kumpenda na kuendelea kumpenda mke wako haijengwi ktk hisia za mapenzi bali katika upendo wa Mungu na hiyo ni kusema kuwa Mke ni kitu cha thamani kuliko mapenzi.


Ndoa bora inajenga Taifa bora,kwa hiyo ustawi wenu katika ndoa yenu ni baraka kwa Ulimwengu wote,mheshimu mke wako kwa nguvu zako zote,mfanye ajisikie ni wa thamani kila siku, mpe fikra yako na thamani yako,ili watoto wenu waone na kujifunza kwenu,kwani watoto wetu wana jifunza zaidi kwa kuona kuliko ushauri.

Kuwa baba na mama mwema ni uchaguzi mzuri,marafiki zetu wanao husika na familia zetu lazima wawe wana tabia njema,kujenga familia chanya na yenye adabu kuna husika sana na watu wanao tuzunguka,ni vizuri kuwa na mahusiano(relationship) na watu wengi lakini kuwa na ushirika(fellowship) kwa ajili ya familia na ustawi wake kuna hitaji hekima.

Kuna wakati nafikiri kuwa kazi zetu za siasa zina tufanya tukose muda mwingi na familia,lakini nimekuja kugundua kuwa sio siasa inatufanya kukosa muda na familia lakini kukosa vipaumbele (lack of priority) juu ya familia ndilo tatizo kubwa.Unaweza ukawa mwanasiasa na familia yako isikukose,kwani to spend money with your family sio muhimu kama to spend time with your family.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Umenibariki sana kaka kwa hekima hii ya kiroho.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad