Ulaji wa Samaki umeshuka Tanzania
0
September 26, 2019
Naibu Waziri wa mifugo na uvuvi, Abdallah Ulenga, amesema kiwango cha ulaji wa Samaki kwa watanzania kipo chini, licha ya taifa kuwa na maziwa, mito, bahari na mabwawa ya wafugaji.
Amesema takwimu zinaonesha ulaji wa Samaki kwa mtanzania ni kilo nne kwa mwaka ukilinganisha mapendekezo ya shirika la Afya Duniani (WHO) inapaswa kuwa kilo 20 kwa mwaka.
Rais Magufuli afanya uteuzi mwingine NBS
Kauli hiyo imetolewa Jijini Mwanza jana, wakati wa uzinduzi wa kadi ya uvuvi uliofanywa na Benki ya Posta Tanzania (TPB), na chama kikuu cha ushirika wa wavuvi Tanzania (TPB), na chama kikuu cha ushirika wa wavuvi Tanzania (Chakuwata), baada ya kuingia makubaliano ya kukopeshwa fedha ikiwa na lengo la kurasimisha kundi hilo.
Ulenga ameongeza kuwa takwimu zinaonesha samaki waliovuliwa mwaka jana ni tani 450,000 huku mahitaji yakiwa ni tani zaidi ya 700,000.
Toni Conceicao aahidi ubingwa 2021
Amesema bado haamini takwimu zinazotolewa kwamba sekta ya uvuvi inachangia pato la taifa kwa asilimia 1.7, ikiwa inashika nafasi ya nne, hivyo aliwataka wahusika wa kukusanya takwimu kufanya unyambulisho wa matumizi ya samaki kuanzia minofu yake, mifupa, utumbo mabondo, matamvua na vitu vingine.
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi, amesema ikiwa taasisi za fedha zitasogezwa kwa wananchi itakuwa ni rahisi taifa kupambana na umasikini na kufanikiwa kukwamua jamii kwa pamoja.
Tags