Urusi kuikabidhi India mfumo wa ulinzi wa makombora

Inaripotiwa kuwa nchi ya Urusi itakabidhi India mfumo wa ulinzi wa makombora wa S-400 kati ya miezi 18-19 ijayo.

Siku chache zilizopita viongozi wa India na Urusi waliingia makubaliano yenye kugharimu Dola Bilioni 5 kwa ajili ya ununuzi wa mfumo huo, licha ya Marekani kutisha India na vikwazo dhidi ya ununuzi wa mfumo huo.

Mfumo wa ulinzi wa S-400 unaweza kurusha kombora hadi umbali wa kilomita 400 na kudungua hadi silaha 80 ukilenga makombora mawili kwa kila moja.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad