Usilolijua kuhusu Nandy na kundi la Sautisol

Siku chache baada ya kuachia wimbo wa 'Kiza Kinene' kwa kushirikiana na kundi la Sautisol la nchini Kenya, Msanii Nandy amesema alikuwa na ndoto kufanya kazi na kundi hilo.

Kupitia ukurasa wake Instagram, Nandy amevunja ukimya na kueleza namna alivyokuwa akiota kufanya kazi na Sauti Sol.

Nandy aliweka kipande cha video kinachomuonyesha akiwa kwenye shindano na msanii wa Sauti Sol, Bien akionekana kumsifia.
.
“Ilikuwa ndoto yangu kufanya kazi na kundi la Sauti Sol nakumbuka kipindi hiki nawaza nikishinda niimbe na wewe,” amesema Nandy.

Wimbo wa 'Kiza kinene' unaonekana kufanya vizuri kwenye vituo vya redio na televisheni huku kwenye youtube ukifikisha watazamaji zaidi ya 700,000 ndani ya siku tatu tangu video itoke.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad