Uwanja mkubwa wa kimataifa wa ndege China wafunguliwa
0
September 25, 2019
Uwanja mpya mkubwa wa ndege wa kimataifa China wenye thamani ya $11bn umefunguliwa siku chache kabla ya maadhimisho ya miaka 70 nchini humo.
Uwanja wa ndege wa Daxing uliopo katika mji mkuu Beijing umefunguliwa rasmi na rais Xi Jinping hii leo.
Una ukubwa wa mita 700,000 mraba - wenye ukubwa wa viwanja 98 vya soka linasema shirika la habari China Daily.
Uwanja uliopo hivi sasa Beijing ni wa pili wenye shughuli nyingi duniani baada ya ule wa Atlanta, kwa mujibu wa wa baraza la viwanja vya ndege.
lakini maafisa wanasema uwanaj mpya wa ndege unahitajika kuondsha shinikizo kutoka kwenye uwanja huo wa kimataifa Beijing unaojaa watu kupita kiasi.
'
Aliyefunga kilo 25 za dhahabu kwenye mapaja akamatwa uwanja wa ndege
Kwa Picha: Kituo kipya cha uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Tanzania
Uwanja wa ndege wa Daxing- unaotajwa kuwa na kiingilio kikubwaduniani katika jengo moja - unatarajiwa kuwapokea idadi kubwa ya wasafri milioni 170 wanaotarajiwa kukaribishwa mjini humo kufikia 2025.
Kwa mujibu wa shirika la serikali, Global Times, ndeg saba za ndani zilitarajiwa kuanza shughuli katika uwanja huo mpya hii leo Jumatano. ndege ya kwanza - China Southern Airlines A380 - iliondoka mwendo wa saa 16:23 kwa saa ya huko.
Na ndege za kimataifa zikiwemo British Airways, Cathay Pacific na Finnair tayari zimetangaza njia mpya kwenda Daxing.
Uwanja huo wa ndege, ulio takriban 46km kusini mwa Tiananmen Square, uliundwa na msanifu mijengo maarufu Zaha Hadid.
Kutokana na ufunguzi huo, Beijing imejiunga na makundi ya miji yakiwemo New York na London, ambayo ina viwanja viwili vya kimataifa.
zaidi ya abiria milioni 100 wamewahi kupitia Beijing Capital, uliofunguliwa mnamo 1958.
Tags