Vurugu zaanza tena dhidi ya mali za wahamiaji Afrika Kusini

 

Mamia ya watu wamekuwa wakionekana wakikimbia na kupora mali za watu katika eneo lenye shughuli za kibiashara na kuchoma moto maduka yanayoaminiwa kumilikiwa na wahamiaji kutoka mataifa ya Afrika. 


Ghasia hizo zilianzia katika eneo la Jeppestown, lililopo katika wilaya ya kati yenye shughuli za biashara. Lakini zilisambaa hadi kwenye maeneo mengine kama vile Denver, Malvern, Turffontein, Tembisa na maeneo mengine ya vitongoji vya jiji la Johansburg. 


Watu 41 wamekamatwa katika wimbi hilo la ghasia. 


Video iliyosambazwa kwa kiasi kikubwa kwneye mitandao ya kijamii inayoonyesha magari kadhaa yaliyoungua kwa moto katika kile kinachoonekana kama mahala panapoegeshwa magari makuu kuu. 


polisi wamefyatua mabomu ya kutoa machozi , na risasi za plastiki kujaribu kusitisha uporaji. 


Msemaji wa polisi Kapteni Mavela Masondo amesema kuwa maafisa wa polisi wamekuwa wakikabiliana na moto katka jengo lililotekwa mjini Jeppestown Jumapili. 


Amesema kuwa watu 3 walikufa katika moto huo, huku mtu wa nne akipata matibabu baada ya kuvuta hewa ya moshi. 


"Wakati bado tunafanya uchunguzi na huduma za dharura , watu waliokuwepo karibu walianza kutumia fursa ya hali iliyopo na kupora maduka." 


Luteni Generali Alias Mawela ambaye ni kamanda wa polisi wa jimbo amesema kuwa polisi wamewakamata walau watu 


katika kile alichokielezea kama ghasia kubwa. 


Haijabainika ni akina nani walioanzisha mashambulio hayo. 


Waziri wa polisi Bheki Cele aliyetembelea eneo la ghasia amelaani ghasia hizo ambazo amesema hazina maana. 


"Wakati bado tunafanya uchunguzi na huduma za dharura , watu waliokuwepo karibu walianza kutumia fursa ya hali iliyopo na kupora maduka ." 


Baadhi yawatumiaji wa mitandao ya kijamii nchini humo wamekuwa wakishirikishana picha na video za ghasia hizo. Mfano Katika picha hii VHo MPHO anaonyesha picha ya eneo la Bree akisema ni krismas katika mtaa huo 


Awali aliashiria kuwa kuna kikundi kikubwa cha watu kinachoelekea katikati mwa jiji na wanasomba kila wanakiona njiani. 


Wengi miongoni mwa watu 41 waliokamatwa walipatikana na mali walizopora wakiwa wamezibeba mapema jumatatu alfajiri. 


Washukiwa wanane walikamatwa ndani ya duka moja 


Kamishna wa polisi wa jimbo la Gauteng Luteni Generali Elias Mawela alielezea matukio haya kama ya ''ukiukaji wa sheria'' na ''yasiyo ya kibinadamu'' 


"Ni siku ya huzuni wakati watu wanapoamua kutumia matatizo ya wengine kwa ajili ya kuendeleza ukiukaji wa sheria au uhalifu . 


Mawela amewaonya watu dhidi ya kuendelea kuchochea ghasia. 


"wale wanaotaka kuibadilisha Gauteng kuwa mahala pa uhalifu watapatikana na watakabiliana na mkono wa sheria ," alisema. 


Ghasia dhidi ya wahamiaji kutoka mataifa ya Afrika ni jambo ambalo si geni nchini Afrika Kusini, licha ya kulaaniwa na maafisa wa usalama na serikali ya nchi hiyo. 


Kundi la wanaume ambao hawana ajira waliwashambulia wahamiaji kutoka Malawi wanaoishi katika mji wa Durban Afrika kusini mwishoni mwa mwezi Machi. 


Ilifuata visa vingine kadhaa katika mji huo katika kipindi cha mwezi huo, jambo lililochangia viongozi kutoka vyama vitatu vikuu kushutumua mashambulio dhidi ya raia wa kigeni.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Dah! UBAGUZI SI KITU CHEMA!
    Walibaguliwa nao sasa wanawabagua wengine tena waafrika wenzao!

    ReplyDelete
  2. Dah! UBAGUZI SI KITU CHEMA!
    Walibaguliwa nao sasa wanawabagua wengine tena waafrika wenzao!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad