Waandamana kupinga muswada unaodhibiti kushiriki ngono kabla ya ndoa
0
September 25, 2019
Makundi ya watu wameandamana nje ya bunge la Indonesia kupinga pendekezo juu ya sheria mpya itakayozuia kushiriki tendo la ndoa kabla ya kufunga ndoa.
Muswada huo unaharamisha ngono kabla ya ndoa kuwa ni kosa la jinai na mhusika anaweza kufungwa mwaka 1 jela, pia kwa wale wapenzi wanaishi pamoja nje ya ndoa muswada huo ukipitishwa inaweza kuwasababishia kifungo cha miaka 6 jela
Hivyo Polisi nchini humo waliamua kupiga mabomu ya machozi kutawanyisha maandamano hayo yaliyofanyika nje ya bunge hilo.
Mswada huo pia unaharamisha kisheria aina nyingi za utoaji mimba ambapo muhusika atafungwa miaka minne jela iwapo hatakutwa na sababu za kimataibabu zilizopelekea mimba hiyo kutolewa au sababu za ubakaji.
Mshtakiwa aomba kujidhamini adai sehemu zake za siri zimetoweka
Lakini pia kuna muswada wa kumtukana Rais, Makamu wa Rais, kiongozi wa dini, taasisi za serikali na nembo kama vile bendera na wimbo wa taifa itakuwa ni moja ya ukiukaji wa sheria.
Mswada huo umekuwa ukicheleweshwa, lakini waandamanaji wanahofu kuwa inaweza hatimae kupitishwa na bunge.
Awali muswada huo ulipangiwa kupigiwa kura Jumanne- lakini rais Joko Widodo aliahirisha kura hadi Ijumaa, akisema kuwa sheria hiyo mpya inahitaji kuchunguzwa zaidi
Licha ya kucheleweshwa kwa kura hiyo, Waindonesia wengi wanahofia kwamba muswada huo unaweza kupitishwa na bunge na hivyo kuwazuwia ”haki zao”.
Aidha wanahasira juu ya kupitishwa kwa sheria mpya inayodhoofisha mamlaka ya tume ya kupambana na ufisadi , ambayo ni muhimu katika juhudi za kumaliza rushwa
Tags