Waasi wa Houthi Wakiri Kuhusika na Shambulio la Vituo vya Mafuta Saudi Arabia
0
September 15, 2019
Ndege zisizokuwa na rubani ambazo waasi wa Houthi wamekiri kuzimiliki zimeshambulia eneo kubwa la kutengenezea mafuta nchini Saudi Arabia pamoja na eneo kubwa la mafuta linalomilikiwa na kampuni ya mafuta ya Aramco nchini humo na kusababisha moto mkubwa katika eneo muhimu la kusafirisha mafuta duniani.
Mpaka sasa haijawa wazi iwapo kuna majeruhi wowote katika shambulio hilo kwenye vituo vya mafuta vya Buqyaq na Khurais, au kujua ni athari za aina gani zitatokea katika shughuli za kuchimba mafuta nchini Saudi Arabia.
Shambulio hilo linaonekana kuongeza mvutano katika Ghuba ya Uajemi kutokana na mkwaruzano uliopo kati ya Marekani na Iran juu ya makubaliano yake ya nyuklia na mataifa yaliyo na nguvu duniani.
Waasi wa Houthi wanaungwa mkono na Iran katika mapambano ya zaidi ya mwaka mmoja dhidi ya kundi hilo mjini Yemen yanayofanywa na muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia.
Tags